21 Juni 2025 - 15:19
Umati wa Wananchi wa Malaysia wameandamana kuonyesha sapoti yao kwa Iran mbele ya Ubalozi wa Marekani Mjini Kuala Lumpur

Hivi karibuni Dunia itashuhudia Haki ikiishinda batili na Imani ikishinda ukafiri.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wananchi wa Malaysia, wamefanya Maandamano makubwa mbele ya Ubalozi wa Iran Mjini Kuala Lumpur kuonyesha sapoti yao kwa Iran. Waandamaji hao, wamelaani vikali Utawala haram wa kizayuni na Uungaji mkono wa Marekani kwa Utawala huo wa jinai na uhalifu.

Ikumbukwe kuwa Israel ni Taifa Ghasibu linaloendelea kuikalia kimabavu Palestina na kumwaga damu za Wapalestina na kuchukua Ardhi zao kinyume na haki. 

Hivi sasa Utawala huo wa Kizayuni umejichanganya kuanzisha vita visivyo vya haki dhidi ya Iran na sasa wanajuta baada ya Majibu ya Kisasi ya Iran, jambo ambalo hawakutegemea itakuwa hivyo. 

Hivi sasa wameanza kuomba Msaada wa Marekani kwamba awasaidie kuingia vitani na Iran ili kuikoa israel. 

Hivi karibuni Dunia itashuhudia Haki ikiishinda batili na Imani ikishinda ukafiri.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha